Home FEDHA Matumizi huduma rasmi za fedha Tanzania kufika 85% ifikapo 2028

Matumizi huduma rasmi za fedha Tanzania kufika 85% ifikapo 2028

0 comment 32 views

Tanzania imejiwekea shabaha kufikia mwaka 2028 kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha kifike 85%.

Tafiti ya Finscope ya mwaka 2023, inaonesha kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha nchini kiliongezeka hadi kufikia asilimia 76.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba ameeleza hayo alipokutana na ujumbe wa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (International Finance Cooperation -IFC) Septemba 10, 2024 katika ofisi za BoT jijini, Dar es Salaam.

“Tumejiwekea shabaha kufikia 2028 kiwango cha utumiaji wa huduma rasmi za kifedha kifike asilimia 85 na uwezekano wa kufikia malengo hayo ni mkubwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ikiwemo usambazaji wa intaneti nchini kote kupitia mkongo wa Taifa ambao utarahisisha huduma za kifedha kwa njia ya mtandao nchini kote,” amesema Gavana Tutuba.

Ameongeza kuwa ili kukuza sekta ya biashara nchini, serikali imefanya jitahada mbalimbali za kuzirasimisha kwa lengo la kuziwesha biashara hizo kwa lengo la kuzikuza na kupunguza uwepo wa biashara zisizo rasmi.

Aidha, Gavana Tutuba ametoa wito kwa IFC kuwekeza katika sekta binafsi nchini kutokana na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

“Tumekuwa tukiwahimiza muwekeze kwenye sekta binafsi nchini kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo,” amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya IFC kwa Ukanda Afrika Mashariki, Mary Peschka, ameishukuru BoT kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali katika kusimamia uchumi wa nchi na ameahidi kuwa IFC itaendelea kushirikiana na Benki Kuu pamoja na serikali kiujumla kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Mkurugenzi wa Taasisi ya IFC kwa Ukanda Afrika Mashariki, Mary Peschka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter