Home FEDHAMIKOPO Elewa mikopo kabla hujakopa

Elewa mikopo kabla hujakopa

0 comment 93 views

Ukikopa fedha, ni muhimu kufahamu jinsi mikopo inavyofanya kazi. Kuwa na ufahamu kuhusu mikopo husaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu madeni, ikiwa ni pamoja na wakati wa kuepuka madeni hayo. Hivyo jifunze jinsi mikopo inayofanya kazi kabla ya kukopa.

Gharama

Inachukua nini kupata fedha? Fedha zaidi. Ukikopa unatakiwa kulipa kiasi cha fedha ulichokopa pamoja na riba. Unaweza pia kulipa na ada. Gharama ni sehemu muhimu ya kuelewa jinsi mikopo inavyofanya kazi na kuchaguamkopo unaokufaa. Kwa ujumla ni muhimu kupunguza gharama. Lakini si rahisi kuelewa kuhusu gharama kila wakati. Wakopeshaji mara nyingi hawaonyeshi kila kitu kuhusu mikopo inayofanya kazi na kwa gharama zipi, ni muhimu ukifanya uchunguzi wako mwenyewe.

Kwa mikopo mingi unashauriwa kutumia jedwali (Spread sheet) ili kujua nini kinatokea ukibadilisha vigezo. Gharama zinaweza kuchanganya, hakikisha unazingatia viwango vya riba na ada unapojifunza kuhusu mikopo.

Kulipa mkopo

Ni mkopo kama utaulipa baadae. Utakapojifunza jinsi mikopo inavyofanya kazi utaona mikopo mingi hulipwa hatua kwa hatua kwa muda fulani. Malipo ya mwezi yamegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kulipa gharama mkopo na sehemu ya gharama za riba yako. Jedwali la uhamishaji huonyesha jinsi hiyo kazi inavyokwenda na jinsi gharama za riba zinavyopungua baada ya muda.

Mkopo unaweza kuwa na muda au usiwe na muda ambao unatakiwa kuulipa. Baadhi ya rehani (Morgages) huchukua miaka 30 kulipa na mikopo mingine huchukua miaka 3. Kadi  ya mkopo ni mkopo unaozunguka, unaweza kulipa mara nyingi uwezavyo bila kuomba mkopo mpya. Makubaliano ya muda mfupi huhitaji malipo makubwa.

Sifa za kupata mkopo

Ili kupata mkopo unatakiwa kuwa na sifa. Wakopeshaji hutoa mikopo pale tu wakijua wanaweza kulipwa. Kadi yako ya mikopo ni muhimu kwani itakuonyesha uliyotumia mikopo yako iliyopita. Mikopo iliyopita mizuri itakuwezesha kupata mkopo kwa kiwango kinachoridhisha. Unaweza pia kuonyesha kwamba una kipato kizuri cha kuweza kulipa mkopo.

Kama huna historia yenye nguvu kuhusu mikopo au unataka kukopa kiasi kikubwa che fedha  unaweza kupata mkopo kwa dhamana. Hii inamruhusu mkopeshaji kuchukua kitu na kukiuza kama utashindwa kurudisha mkopo. Huenda hata mwenye mkopo mzuri zaidi yako mnaweza kushirikiana kukopa, ukishindwa kulipa huyo mtu mwingine anatakiwa kukubali kulipa baada yako. Wakati mwingine, uandishi mzuri wa ombi la mkopo pia husaidia

Jinsi mikopo inavyofanya kazi

Sasa unajua zaidi kuhusu kukopa kwa ujumla. Lakini je mikopo inafanyaje kazi katika maisha ya kila siku? Unapotaka kukopa, unaenda kwa mkopeshaji na kuomba mkopo. Benki yako au muungano wa mikopo ni sehemu nzuri ya kuanzia. Unaweza kufanya kazi na wakopeshaji maalumu kama madalali wa mikopo na watoa huduma ya mikopo.

Baada ya kutoa taarifa zinazokuhusu, mkopeshaji atapitia maombi yako na kuamua kama unafaa au hufai kupewa mkopo. Akiridhia mkopeshaji atakutumia fedha hizo (au atatuma kwa mtu mwingine moja kwa moja: kwa mfano kwa mtu ambae unataka kununua nyumba kwake. Baada ya muda mfupi wa kupokea fedha hizo utaanza kulipa kidogo kidogo kwa kawaida baada ya mwezi.

Ikiwa unataka kuokoa fedha, unaweza kulipa mikopo mapema kwa ujumla. Fahamu jinsi mkopo wako unavyofanya kazi kama kuna malipo yanatakiwa kufanywa kabla na hakikisha inaleta maana kabla ya kufanya hivyo.

 

Imeandikwa na Justin Pritchard na kutafsiriwa na Leah Nyudike.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter