Home FEDHAMIKOPO Mamilioni yanufaisha vikundi 48

Mamilioni yanufaisha vikundi 48

0 comments 174 views

Kufuatia agizo la kila Halmashauri hapa nchini kutenga na kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye walemavu, mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 198 imetolewa kwa vikundi 48 katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Juma Mnwele amesema kuwa wametoa mikopo hiyo kwa lengo la kuwainua walengwa kiuchumi na kutekeleza agizo la serikali. Mnwele ameeleza kuwa kwa mwaka 2016/17 hadi 2018 Halmashauri hiyo imetoa milioni 20 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Akizungumzia suala la vitambulisho kwa wajasiriamali, Mkurugenzi hiyo amesema Halmashauri inaendelea kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali ili wasisumbuliwe katika shughuli zao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ambrose Nchimbi amesema wataendelea kukusanya mapato na kutoa mikopo ili kuboresha maisha ya wananchi. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbinga, Beda Hyera ametoa pongezi kwa Halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo hilo ikiwa ni moja ya mambo ambayo yamelenga kuinua wananchi na kuchochea maendeleo.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye amesema kutokana na utaratibu huo wananchi wengi wataondokana na umaskini. Ametoa wito kwa makundi hayo kurudisha fedha hizo kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!