Home FEDHA Sababu 4 hutakiwi kuweka fedha na mwenza wako

Sababu 4 hutakiwi kuweka fedha na mwenza wako

0 comment 99 views

Siku zote watu wakiwa katika mahusiano hufanya mambo mengi pamoja lakini suala la fedha linakuaje? Je, kuna umuhimu wa kuweka fedha pamoja? Watu wengi huweka fedha pamoja na wenza wao japokuwa hii inaweza kuwa sio njia sahihi kwa kila mwanandoa kwani lolote linaweza kutokea na kuathiri mahusiano kwa namna moja au nyingine.

Hizi hapa ni sababu nne ambazo zinaeleza ni kwanini kuna umuhimu wa kila mtu kuweka fedha zake.

Kupunguza ugomvi

Chanzo kikubwa cha ugomvi wa wanandoa wengi ni masuala ya fedha, hasa kama kuna vipaumbele tofauti na kila mmoja wao ana njia tofauti za kuweka akiba na matumizi. Kuweka fedha tofauti kuNasaidia kupunguza malumbano baina ya wanandoa kwa sababu kila mmoja anakuwa na uhuru na fedha zake. Pia kwa kuweka fedha tofauti kunakuwa hakuna desturi ya kuomba ruhusu kutumia fedha kwa ajili ya matumizi mbalimbali hususani matumizi binafsi.

Husaidia kutunza uhuru wa kifedha

Wenza wanapoweka fedha pamoja, mtu mmoja huchukua majukumu ya usimamizi wa fedha hizo hali inayoweza kuleta utata katika matukio kama kifo, talaka, magonjwa nk. Kwa kutenganisha fedha kila mtu anakuwa na uhakika mambo hayatabadilika ikiwa matatizo kama hayo yatatokea.

Ni rahisi kusimamia majukumu ambayo tayari yapo

Mara nyingi watu wakiingia katika uhusiano huwa na majukumu tofauti kama vile watoto, mikopo ya biashara, madeni ya chuo nk ikiwa kila mmoja ataweka fedha zake, inakuwa rahisi kufanya malipo hayo bila ya kumuelemea mwezi wako.

Huleta mawasiliano zaidi kuhusu fedha

Kwa kuweka fedha tofauti ni rahisi kuongelea masuala ya kifedha na mwenza wako ili kuhakikisha maisha yanakwenda vizuri na kila mtu anafanikisha malengo yake. Mnapoweka fedha pamoja, ni rahisi kwa pande moja wapo kuwa na visingizio kila wakati kuwa hana fedha ya ziada lakini kwa kuweka fedha tofauti inakuwa rahisi kuwasiliana mapema kuhusu mambo yanayotakiwa kufanyika ili kupeana muda kutafuta fedha na kuweza kutimiza majukumu.

Mwisho wa siku, ni wewe tu unayeweza kuamua maamuzi yapi ni sawa kwako. Jambo la msingi ni kufanya mazungumzo ya kina na mwenza wako ili kufikia muafaka wa nini kifanyike kuweza kuepuka ugomvi, kuwasiliana zaidi kuhusu malengo na mtiririko wenu wa fedha.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter