Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu amewataka wananchi kuangalia tozo wanazokatwa na mabenki na makampuni ya simu badala ya kulalamikia makato ya serikali.
Akizungumza Bungeni Septemba 21, 2022, Zungu amesema “mimi niwaombe wananchi pamoja na sisi wabunge, unapotuma pesa tizama breakdown(mchanganuo) ya pesa inavyoandikwa, utaona tozo ya serikali ipo chini sana na mapato wanayochukua makampuni ya simu na taasisi za fedha yapo juu zaidi ya mapato inayopata serikali”.
Amesema mabenki yanachukua pesa kubwa zaidi ya serikali kwa asilimia kubwa lakini Serikali inayojenga madarasana na vituo vya afya ndio inayolaumiwa.
Amesema jambo hilo linatakiwa kuangaliwa ni namna gani mabenki na kampuni za simu wanaweza kupunguza gharama za huduma zao.
Soma zaidi: Serikali ya Tanzania yafuta tozo miamala ya kieletroniki