Home FEDHA TRA: Hakuna aliyehujumu mfumo wa kulipa kodi

TRA: Hakuna aliyehujumu mfumo wa kulipa kodi

0 comment 116 views

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo amesema mfumo wa kulipa kodi kwa njia ya kielektroniki haujahujumiwa kwa namna yoyote na hakuna upotevu wa mapato ya serikali. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Kayombo ameeleza kuwa, maboresho ya kiufundi yanaendelea hivi sasa katika mfumo huo ili kuhakikisha kuwa unatimiza malengo yaliyokusudiwa. Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa, katika kipindi hiki ambacho maboresho yanaendelea, kampuni mbalimbali zikiwemo za simu pamoja na benki zinaendelea kulipa kodi kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa hakuna upotevu wa aina yoyote wa mapato kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti.

“TRA inapenda kuuhakikishia umma kwamba hakuna ofisa wa serikali mwenye nia ya kuhujumu mfumo huo kwa lengo la kujinufaisha na kuzorotesha juhudi za serikali za ukusanyaji mapato, bali kuna maboresho ya kiufundi yanaendelea kwenye mfumo huo hivi sasa, lakini uko salama na hakuna upotevu wowote wa mapato”. Imeeleza taarifa hiyo.

Mbali na hayo, Kayombo amesema umebaki mwezi moja pekee kufika mwisho wa kupokea maombi ya msamaha wa riba na adhabu kwa asilimia 100 katika malimbikizo ya kodi na kwamba, mara baada ya muda huo kuisha mamlaka hiyo haitatoa muda wa nyongeza na badala yake wahusika watalazimika kulipa malimbikizo yote pamoja na riba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter