Home BENKI KCB Tanzania yatoa msaada Amana

KCB Tanzania yatoa msaada Amana

0 comment 118 views

Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wa thamani ya Sh. 6 milioni kwa wodi ya wanawake hospitali ya rufaa ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mahusiano wa KCB Tanzania, Christine Manyenye amesema  kuwa mchango huo ni moja kati ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji wa masuala ya kijamii ili kuwasaidia wale walio na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya afya, elimu, mazingira, ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”. Amesema Manyenye.

Manyenye ameeleza kuwa benki ya KCB imetoa misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20 vyote vikiwa na thamani ya Sh. 6,017,000 na kuongeza kuwa upungufu wa vitanda, magodoro na mashuka katika hospitali nyingi nchini imekuwa changamoto hasa katika wodi za wakina mama na watoto, hali iliyopelekea benki hiyo kuamua kutoa msaada ili kupunguza changamoto hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Amana, Dr. Amim Kilomoni ameishukuru benki ya KCB kwa msaada huo na kusema utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili, ikiwemo upungufu wa vitanda, magodoro pamoja na mashuka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter