Home FEDHA Uingereza yatoa msaada wa Trilioni Moja

Uingereza yatoa msaada wa Trilioni Moja

0 comment 92 views
Na Mwandishi wetu

Uingereza imetoa msaada wa Dola za marekani milioni 450 ambazo ni sawa na trilioni moja za kitanzania ili kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Msaada huo umetangazwa na Waziri na Nchi Maendeleo ya Kimataifa na masuala ya Afrika katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola, Rory Stewart baada ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam.

Fedha hizo zinategemewa kusaidia maeneo mbalimbali ya maendeleo hasa kuinua elimu na kuongeza idadi ya watoto wanaopata elimu. Pia zitatumika kuboresha miundombinu kama barabara na bandari, kuinua kilimo cha biashara na viwanda vya pamba na nyama. Waziri huyo amesema serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali, ameongeza kuwa ana imani msaada huu utainua uchumi na maisha ya watanzania.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amemshukuru Stewart na serikali ya Uingereza kwa msaada huo mkubwa waliotoa na kumhakikishia kuwa serikali yake inatambua mchango mkubwa wa nchi hiyo katika maendeleo ya taifa letu. Mbali na hayo, amekumbusha watanzania kulipa kodi kwani ni kitu muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter