Home FEDHA Usimamizi ‘madhubuti’ mapato kila mkoa ni muhimu

Usimamizi ‘madhubuti’ mapato kila mkoa ni muhimu

0 comment 91 views

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa  na Serikali za mitaa(Tamisemi) Joseph Nyamhanga, amewasisitiza  makatibu tawala nchini kuisaidia serikali ipasavyo katika suala zima la ukusanyaji na usimamizi wa mapato katika mikoa yao.

“Usimamizi wa fedha za umma ni eneo muhimu sana katika mamlaka ya serikali za mitaa, hivyo tumewaita ma-ras wote  na wataalamu ili waweze kusimamia vizuri mpango wa maboresho  ya usimamizi wa fedha  za umma katika mamlaka za mikoa na serikali za mitaa” amesema Nyamhanga.

Katibu huyo amesema ili kutimiza mpango huo wa miaka mitano  makatibu tawala wanatakiwa kujua habari zote zinazohusu  fedha zinazokusanywa,zinazotoka, na zile  zinazotoka kwa wadau wa maendeleo, na kuwataka ma-ras kuhakikisha vitengo vya ndani vya usimamizi viko imara ili kuepukana na changamoto zozote. Akaongezea kuwa kuna umuhimu wa kuwa usimamizi imara kwenye masuala ya manunuzi ili sheria ziwezwe kufuatwa ipasavyo.

Mwakilishi wa wadau wa maendeleo ambao kupitia DFID ni miongoni mwa wanaochangia mpango huo Oliver Blake, amesema ni muhimu watumishi wengine kuiunga mkono Serikali ili kukamilisha mpango huo na kwamba hadi sasa wadau wa maendeleo wanalidhishwa na operesheni inayofanywa na serikali ili kutimiza mpango huo. Hivyo kupitia mikutano itakuwa rahisi kujadili vikwazo na namna ya kutatua vikwazo hivyo ili kukamilisha mpango huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi anaeshughulika na fedha za serikali za mitaa, Shomari Mukhandi, amesema kuwa mpango huo una manufaa makubwa kwani mwaka 2017/18 walipanga kukusanya mapato ya Shilingi bilioni 687 na mwaka huu wanategemea kukusanya Shilingi bilioni 735.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter