Home FEDHABIMA Kampuni za bima zatakiwa kuelimisha jamii

Kampuni za bima zatakiwa kuelimisha jamii

0 comment 61 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango, ametoa wito kwa taasisi za bima nchini kubuni mbinu mbadala ya kutoa elimu kwa umma ili kuwafikia wananchi wote wakiwemo wakulima na wafugaji ili kuwapa nafasi ya kutambua umuhimu wa kuwa na bima. Waziri Mpango amesema hayo mkoani Tanga katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa bima ulioandaliwa na taasisi ya umoja wa  makampuni ya bima. Dk. Mpango amedai kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana utaratibu wa kuwa na bima, sababu kubwa ikiwa ni ukosefu wa elimu kuhusu umuhimu wa bima. Waziri huyo ameagiza taasisi za bima kuweka mpango rafiki wa elimu utakaowagusa watanzania wote.

“Kuwa na bima ni muhimu kwa kuwa inasaidia kutukinga na majanga yanayoweza kutokea wakati wowote kama mlivyoona kwa watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv. Nyerere, hawakuwa na bima jambo lililosababisha Rais John Magufuli kuona huruma na kutoa shilingi milioni moja kwa kila marehemu”. Amesema Dk. Mpango.

Kwa upande wake Kamishna wa bima nchini Dk. Baghayo Saqware amefafanua baadhi ya mikakati yao kwa mwaka 2018 hadi 2020  na kudai wamalenga kuwafikia wananchi zaidi kwa kutoa elimu ya bima kuanzia ngazi za mitaa na kupitia wajasiriamali wadogo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter