Home FEDHA Zitambue faida za kuweka Akiba

Zitambue faida za kuweka Akiba

0 comment 195 views

Mambo mengi unayopanga kuyafanya katika kipindi chote cha maisha yako yanahitaji Pumzi Afya na Fedha. Hivi unakumbuka mala ngapi ulijaribu kuweka fedha, ukashindwa au ukazitumia kabla ya kutimiza malengo. Huenda ulikuwa hufahamu faida za kkuweka Akiba.

Watu wengi hufikilia ili kuweka akiba unatakiwa uwe na pesa nyingi za ziada. Lakini ukweli ni kuwa kuweka fedha ni maamuzi ya mtu.

Sasa basi leo tumewaletea faida tano za kuhifadhi fedha.

Kujikinga na dharura

Dharura ni jambo ambalo hutokea bila ya taarifa. Kipindi cha dharura watu wengi hulazimika kuingia kwenye madeni wasiyoyatarajia. Hivyo kwa kujiwekea akiba kutakuepusha na madeni wakati wa dharura kama msiba, ugonjwa na mengineyo.

Kuwa na nidhamu ya Fedha.

Kuweka akiba kutakusaidia kuwa na nidhamu ya pesa yako. Ukiwa unapata Sh.20,000 kwa siku, itakubidi uitumie vizuri ili kuweza kuweka fedha ya akiba yako.

Kama huna utaratibu wa kuweka akiba ya fedha hutoweza kuwa na nidhamu ya fedha unayopata.

Hukuwezesha kuandaa kesho yako vyema

Maandalizi ya kesho yanafanywa leo. Kuweka akiba maana yake unajiandaa kwa mahitaji ya kifedha ya baadaye — yaani kesho. Mtu asiyeweka akiba mara nyingi hafikiri kuhusu kesho wala hana malengo kwa ajili ya baadaye yake.

Ili kujenga baadaye au kesho njema, ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba.

 

Kuwa na uhuru wa kifedha

Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani.

Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha, ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi.

Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha.

Kupunguza hofu

Unapokuwa huna akiba yoyote unakuwa na hofu juu ya maisha yako. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje? n.k.

Unapokuwa na akiba yako huna haja ya kuwa na hofu kwani unajua hata ukipata taizo akiba yako ipo itakusaidia.

Mwisho

Uwekaji wa akiba ni suala linalohitaji kujitoa na kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Pia kumbuka kuweka fedha huku ukiwa na malengo nayo. Mfano unaweza kuweka akiba kwa ajili ya Biashara, ujenzi, kujiendeleza na elimu na mengineyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter