Rais John Magufuli wa Tanzania ametoa wito kwa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuzishawishi nchi zao kutumia fedha za ndani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia EALA mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.
Pamoja na wito huo pia amesisitiza kuwepo na viwanda vya kuzalisha bidhaa ambazo zitatumika hapa hapa badala ya kutegemea bidhaa na misaada kutoka nje ya nchi. Rais Magufuli pia amezitaka nchi hizo kujenga miradi mikubwa kama vile miundombinu kwa kushirikiana na kutumia uzoefu wa nchi moja na kupeleka katika nchi nyingine.
Mbali na hayo, ameshauri nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujiamini katika uwezo wao wa kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za ndani. Vilevile ameagiza bidhaa kuzalishwa na nchi za jumuiya na kutumika kwa kuwa malighafi zote muhimu zinapatikana