Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Balozi Amina:Wajasiriamali waendelezwe

Balozi Amina:Wajasiriamali waendelezwe

0 comment 96 views

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali amesema wajasiriamali wadogo wanatakiwa kuendelezwa ili kukuza uchumi. Balozi  Amina amesema hayo alipokuwa akizindua Bodi ya Wakala wa Usimamizi wa Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa (Smida) ofisini  kwake eneo la Migombani mjini Unguja.

Balozi Amina alisema kuwa iwapo wananchi wenye umiliki wa viwanda vidogo vidogo watatengenezewa mazingira bora ya kufanyia kazi, itasaidia kuwa na viwanda vikubwa vyenye tija kwa wananchi na kuongeza ajira. Ameongeza kuwa, serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira bora kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda.

Mbali na hayo, Baozi Amina ameitaka Bodi ya usajili wa viwanda kushirikiana na mataifa mengine katika uendelezaji viwanda vidogo vidogo ili kupata ujuzi.

Naye Mwenyekiti wa bodi hiyo, Mussa Silima amesema kwa kushirikiana na wajumbe watahakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu ili kuwaletea wananchi maendeleo. Silima ameongeza kuwa, anafahamu wakazi wengi wa Zanzibar wanategemea uwepo wa viwanda vidogo,hivyo kuna haja kubwa ya serikali kusimamia na kuhakikisha wanayatimiza malengo yao.

Aidha kutokana na kutokuwepo kwa viwanda vikubwa visiwani humo, Silima ametoa wito kwa wawekezaji kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter