Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI ELIMU NA UJASILIAMALI,JE VYOTE VINAWEZEKANA?

ELIMU NA UJASILIAMALI,JE VYOTE VINAWEZEKANA?

0 comment 130 views

Maisha ya mwanafunzi ambaye ni mjasiriamali ni magumu. Ni changamoto kutenga muda kwa ajili ya masomo wakati kuna wateja ambao unatakiwa kuwahudumia. Licha ya yote hayo, kuwa mwanafunzi mjasiriamali ni suala ambalo linawezekana kabisa. Unaweza kuendelea na masomo yako na wakati huo huo kuendesha biashara. Ukiwa mwanafunzi una fursa mbalimbali za kujifunza na kuboresha huduma unayotoa hivyo ni wakati mzuri wa kujiendeleza na kutimiza malengo yako ya elimu pamoja na biashara.

Kama wewe ni mwanafunzi na pia una biashara, fanya haya ili kuwezesha kila kitu kwenda sawa:

1. Chukua nafasi hii kutafuta fursa mbalimbali za misaada

Tofauti na mikopo, misaada huwa na masharti ambayo siyo magumu hivyo upatikanaji wake ni rahisi kidogo. Chuo/Shule ni mahali ambapo watu wengi hutoa misaada kwa watu ambao ndiyo kwanza wanaanza biashara zao hivyo upo katika nafasi ya kupata fedha ambazo zitakuwezesha kuendesha biashara yako hata baada ya masomo. Kama mfanyabiashara mchanga nafasi hii itakusaidia kufika mbali na kuepuka kuelemewa na madeni tangu mwanzo wa safari yako.

2. Tumia wakati huu kujichanganya na kujenga mahusiano ya kudumu

Ukiwa mwanafunzi ni rahisi zaidi kukutana na watu wa aina mbalimbali na kujenga mahusiano ya muda mrefu. Huu ni muda ambao hutakiwi kukaa nyuma hivyo hakikisha unajichanganya kila nafasi inapotokea. Hudhuria matamasha na vikao kadri uwezavyo. Hakikisha unatengeneza mtandao wa watu wengi ambao baadae wanaweza kuwa wateja wako wakubwa. Mbali na hivyo pia jifunze kwa watu wengine na endelea kujiongeza ili kuhakikisha biashara yako ina muelekeo mzuri tangu mwanzo.

3. Omba ushauri kwa walimu wako

ADVERTISEMENT

Walimu wapo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa unafanikiwa. Baada ya kumaliza chuo/shule sio rahisi kukutana na watu ambao watakupa ushauri na kukuongoza vizuri hivyo huu ni muda wako kuwatumia walimu ipasavyo. Kama una wazo wafuate ili wakupe ushauri na maoni yao, waulize maswali na waombe muongozo mara kwa mara ili uwe na uhakika kuwa upo kwenye njia sahihi. Watu hawa wanapoona na kuelewa malengo yako wanakuwa tayari kukusaidia muda wowote na watafurahia kuona maendeleo yako.

Biashara ni sekta ngumu. Kuwa mwanafunzi nayo sio kazi rahisi. Kuanzisha biashara wakati bado unasoma ni ngumu lakini inawezekana. Upo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa kama utafuata ushauri wa hapo juu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter