Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Unataka kunufaika na kipaji chako?

Unataka kunufaika na kipaji chako?

0 comment 135 views

Imeandikwa na Abdul Kitumbi.

Kipaji ni uwezo wa asili wa mtu , kila mtu anakipaji chake ingawa sio kila mtu anweza kutambua kipaji chake.

Ikiwa utaweza kugundua una kipaji cha aina gani, unaweza kuwa umevumbua rasilimali ambayo inaweza kukusaidia katika maisha yako. Ikiwa unatafuta biashara ya kufungua, au unatataka kutafuta njia ya kukuza biashara uliyonayo, unaweza kupata jibu katika kipaji ulicho nacho.

Njia za kugundua kipaji chako;

Hapo ulipo, Uliza watu 10 kila mmoja kipaji chake ni kipi? Unaweza kupata majibu ya kushangaza wengi wao wanaweza sema hawajui.

Kufahamu Kipaji chako ni rahisi sana tofauti na unavyoweza kufikilia, Hapa chini kuna njia 4 rahisi za kuweza kugundua kipaji chako. Njia hizo ni kama zifuatazo:

Shirikisha watu wako wa karibu

Watu wako wa karibu mara nyingi huwa wa kwanza kugundua kipaji chako. Ukijatafakari utagundua kuna wakati watu hao walikuwa wakikuambia juu ya uwezo fulani ulionao, inawezekana ulikuwa hauiskilizi kwa makini sasa ndio wakati sahihi wa kuwasikiliza.

Amua ni nini rahisi

Je, kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya kwa urahisi sana, wakati wengine hupata shida kuyafanya mambo hayo. Mfano kuchora kucheza mpira, kuimba . Ikiwa umegundua kuna mambo ambayo ni rahisi sana kwako kuyafanya na wengine wanashindwa kuyafanya kwa urahisi, jua mambo hayo huenda yakawa ni moja ya vipaji asilia ulivyo navyo.

Kile unachofurahia zaidi

Kipaji kinaweza kujionesha kwa njia nyingi tofauti tofauti, Je! Kuna mada hupendelea sana kuzifuatilia sana na huwa na furaha sana kuzifahamu? Fikiria  ni vitu gani unapenda sana kufanya ukiwa na muda wa ziada. Na huwa unavutiwa navyo kwa ukaribu zaidi , Jua inaweza kuwa ni moja ya vitu hivyo ni  kipaji chako.

Uliza tu

Muulize kila mtu unayemjua ambae anaweza kukupa majibu kwa uaminifu juu ya kile wanachokiona kinaweza kuwa ni kipaji chako. Mara nyingi watu huzingatia mambo mabaya kuhusu watu lakini hiyo haimaanishi kuwa hawajui uwezo wako hivyo uliza watu wako wa karibu unaowaamini mambo machache wanayoona unauwezo nayo mkubwa ambayo yanaweza kuwa ni kipaji chako. Waulize watu wengi kadri iwezekanavyo, kila mmoja kwa wakati wake tofauti, kisha linganisha majibu yao. Bila shaka lazima utapata jibu moja la kipaji chako.

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter