Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali washauriwa kuchangamkia fursa ATCL

Wajasiriamali washauriwa kuchangamkia fursa ATCL

0 comment 91 views

Baada ya kuwatembelea wajasiriamali wadogo wa bidhaa mbalimbali kama chakula na vinywaji, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amewashauri wajasiriamali hao kutumia fursa za kutangaza bidhaa hizo kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuinua kipato chao.

“Rais wetu ametengeneza fursa hii kwa kulifufua shirika letu la ndege kwa kununua ndege zaidi ya sita, lakini pia ametoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa ndege, hivyo wazalishaji wa bidhaa mbalimbali za vinywaji pamoja na vyakula wanatakiwa kuitumia fursa hii ili waweze kujiongezea kipato”. Amesema Dk. Mahenge.

Dk. Mahenge amesema itakuwa vizuri endapo shirika hilo litaweka bidhaa za ndani pia na sio za nje peke yake hivyo kuwataka wajasiriamali hao kutengeneza bidhaa zenye viwango ili kuweza kuuza katika shirika hilo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa shirika hilo, Josephat Kagirwa amesema azma ya ATCL ni kuona bidhaa za ndani zinauzwa katika ndege za shirika hilo hivyo wanakutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali katika mkoa huo ili kuona bidhaa zinazoweza kuuzwa katika ndege zake.

“Tayari tulishaanza na bidhaa kama vile mvinyo katika ndege zetu, mvinyo unaotumika hivi sasa ni kutoka hapa Dodoma, lakini pia bado zipo huduma ambazo sisi tunazitoa katika ndege zetu kama vile vyakula pamoja na mablanketi kwa ajili ya zile safari za mbali hivyo tumekuja kuziona hizi bidhaa ili tuweze kutoa uamuzi wa kuzitumia”. Ameeleza Kagirwa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter