Home KILIMO Kamati ya PAC yakoshwa ujenzi wa vihenge Manyara

Kamati ya PAC yakoshwa ujenzi wa vihenge Manyara

0 comments 44 views

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na ujenzi wa vihenge vya kuhifadhia mazao na maghala wilayani Babati, Mkoa wa Manyara ambavyo vinasimamiwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

PAC ilifanya ziara Machi 18, 2025, ambapo Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga amesema kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa mradi huo na thamani ya fedha zilizotumika.

“Tumekuja kuona mradi wa vihenge ambapo Kamati imefurahishwa sana na namna vihenge vilivyojengwa, kwani vinaongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kwa manufaa ya Taifa,” amesema Hasunga.

Vihenge hivyo kwa sasa vimehifadhi tani 776,000 za mazao, zikiwemo tani 32,000 za mpunga, tani 400 za mtama (tayari zimechukuliwa) ambapo lengo la Serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kuhifadhi tani milioni 3.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Mweli amesema kuwa miradi hiyo awali ilikuwa imekwama, lakini  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alihakikisha inapata ufadhili ili kuendelea na utekelezaji wake.

“Tumepokea maelekezo ya Kamati na tutahakikisha kuwa vituo vitano vilivyosalia kati ya nane vinakamilika haraka ili wananchi wapate huduma,” amesema Katibu Mkuu Mweli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!