Home KILIMOKILIMO BIASHARA Bashe azitaka nchi za SADC kushirikiana kuzalisha chakula

Bashe azitaka nchi za SADC kushirikiana kuzalisha chakula

0 comment 79 views

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa rai kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kushirikiana kuzalisha chakula kwa mpango ambao kila nchi itanufaika.
Bashe ameyasema hayo Julai 3, 2023 wakati akiwasilisha mada kuhusu kilimo cha kisasa kama njia ya kukabiliana na upungufu wa chakula katika mkutano wa 53 wa Mabunge ya SADC (SADC PF 53) unaofanyika jiji Arusha.

Waziri Bashe amesisitiza kuwa kila nchi izalishe mazao ambayo itawauzia wengine kutokana kwa kutegemea uwezo wa nchi husika wa kuzalisha zao husika.

Ametoa mfano wa uwezo wa Tanzania katika kuzalisha mahindi na mchele ukilinganisha na nchi nyingine za SADC na kusema ni vema nchi nyingine zinunue chakula hicho na Tanzania inunue mazao mengine kutoka nchi wanachama.

Waziri Bashe ameongeza kuwa kwa sasa tishio kubwa linalozikabili nchi nyingi za SADC ukiondoa Afrika Kusini ni upatikanaji wa mbegu, jambo ambalo linaweza kukwamisha jitihada za kuwa na uhakika wa chakula.

Kuhusu njia za kisasa za kuendesha kilimo, Waziri Bashe amesema Tanzania imepanga kuwa na hekta za mraba milioni nane za kilimo cha umwagiliaji ifikapo mwaka 2030 ili kujiwekea uhakika wa kuzalisha chakula kipindi chote cha mwaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter