Home KILIMOKILIMO BIASHARA HATUA YA MAENDELEO KWA WAKULIMA,PITIA HII

HATUA YA MAENDELEO KWA WAKULIMA,PITIA HII

0 comment 147 views

Miezi michache iliyopita, kampuni ya utafiti ya BMI ilitoa ripoti yake kuhusu biashara ya kilimo ambapo imebainika kuwa uhitaji wa mazao ya kahawa, mahindi, miwa na mchele utaongezeka maradufu ndani ya miaka michache ijayo. Japokuwa haya ni makadirio tu, hii ni habari njema kwa wadau wa masuala ya kilimo Tanzania. Wakulima na hata wale wanaofikiria kuwekeza katika kilimo wamepewa mwanga na namna sekta hiyo itakavyokuwa miaka michache kuanzia sasa. Hivyo basi wanajiandaa vipi? Ripoti hii itawasaidia kujikwamua na kukabiliana na ushindani sokoni? Vipi kuhusu teknolojia wanayotumia?

Ni vizuri kama wakulima wakijiandaa ili hadi kufikia kipindi ambacho mazao haya yatakuwa  na uhitaji mkubwa kote ndani na nje ya nchi basi wawe tayari. Lakini wao peke yao hawawezi kufanikisha hili. Wanahitaji msaada kutoka serikali kuu pamoja na mashirika mengine yasiyo na kiserikali. Wanahitaji kupatiwa elimu, pembejeo na misaada mengine ya msingi ili wafanikiwe kupata mavuno yaliyo bora na ambayo yatawaletea faida.

Tafiti kama hizi zina umuhimu mkubwa kwa taifa kwani asilimia kubwa ya watanzania wamejiajiri au kuajiriwa kupitia kilimo. Tafiti kama hizi zinawasaidia watu hawa kupata muelekeo. Zinatoa picha halisi ya kipi kinahitajitaka sokoni na kipi hakihitajiki. Huu ni muda wa serikali kutoa ushirikiano na kuangalia namna gani wanaweza kuwasaidia. Jitihada pia zifanyike ili kuhakikisha kuwa hata wale wakulima ambao hawafikiwi na habari muhimu kama hizi wanapata taarifa ili nao pia wajipange.

Wakulima nao waanze kulima kwa faida. Ni wakati wa kuachana na kilimo cha mazoea. Ili kufanya hivyo, wanatakiwa kuwa wafuatiliaji wa masuala ya kilimo, waangalie hali ya soko iko vipi na pia wafuate ushauri wa wataalamu wa kilimo. Watanzania wengi wamekuwa wakifanya kilimo kisicho cha kisasa na hivyo wameshindwa kupata matokeo mazuri. Tafiti kama hizi zinazofanywa zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa wakulima mwanga. Teknolojia nayo inarahisha upatikanaji wa habari kama hizi na kujifunza namna gani unaweza kuboresha kilimo chako. Elimu zaidi inatakiwa kutolewa kwa wakulima kuhusu jinsi ya kutumia mitandao na teknolojia kwa ujumla ili kufanya kilimo bora.

ADVERTISEMENT

Kilimo ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya taifa letu kwani watanzania wengi wanaitegemea kuendesha maisha yao. Wadau wa kilimo wanatakiwa kufanya kazi kwa karibu na wakulima ili kuhakikisha kuwa, kilimo kinafanyika kisasa zaidi na kuwanufaisha watanzania walio wengi. Kilimo bora ni nguzo ya kuwa na viwanda bora na sekta hizi mbili zitasaidia kuinua uchumi wa nchi na kutufikisha mbali kimaendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter