Home KILIMOKILIMO BIASHARA KIJUE KILIMO BORA CHA KATANI AU MKONGE

KIJUE KILIMO BORA CHA KATANI AU MKONGE

0 comment 166 views

KILIMO BORA CHA KATANI AU MKONGE :

UTANGULIZI

Katani ni moja kati ya zao la biashara

Jina la kisanyansi ; Agave sisalana

Jina maalufu ; sisal au katani

Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine nyingi, kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia  India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius na ni zao ambalo hutumika sana kutengenezea bidhaa nyingi.

 

HALI YA HEWA

JOTO LIDI ; Katani hukua vizuri katika maeneo ya kisubtropikia, yaani hukua vizuri kwenye maeneo ya joto yenye joto kati ya 10-32 oC na joto ya juu zaidi inakua 30 hadi 40oC na joto ya hali ya chini zaidi ni 5oC.

MVUA ; Pia mvua huchukua nafasi muhimu katika kilimo cha katani zao hili  huzaa vyema zaidi katika maeneo yenye mvua 500mm na zaidi kwa mwaka na wastani wa mvua 600mm hadi 1500mm na pia huweza kukua kwenye maeneo yenye mvua chini ya hapo.

UDONGO ; Zao la katani halibagui sana udongo lakin hukua vyema kweye maeneo ambayo yana unyevu wa kutosha na aina nyingi za udongo isipo kua udongo mfinyanzi na pH 4.0 hadi 6.0 ni muhimu.

MBEGU : Katani hupandwa kwa kutumia bulbils na suckers

Suckers ; ni vile ambavyo vinakua karibu na mmea na utokana na matokezi (buds) na vinaweza kuchukuliwa na kupandwa moja kwa moja shambani

Bulbils ; Pale katani inapokua huzaa maua katika mlingoti wake, hivi huchukuliwa na kupandwa katika kitalu na watu wengi hupenda kuaanda hivi kwa kua hua na sifa kamili kama ya mmea ambao ni mzazi.

KUANDAA SHAMBA
Mfumo unao hitajika ni ule wa mistari miwili yaani double rows.

Hivyo andaa shamba kwa kulipalilia vizuri na kuondo taka zote.

KUPANDA
Kama nilivyo sema awali bulbils lazima zipandwe kweye kitalu kwanza vinapandwa  10cm x 10cm na hukaa kwenye kitalu kwa mda wa miezi 6 na baada ya hapo huamishiwa tena kwenye kitalu kikubwa ambapo hupandwa kwa 30cm x 30cm ,

Na baada ya miezi 12 hadi 18 mimea hua tayari sasa kwakupandwa katika shamba kubwa na nafasi kati ya mistari hua  ni 1 hadi 1.5 m na 4 m na kina cha kupanda mmea hua ni 3cm  katika kuhamishia shambani mizizi midogo  pembeni ya mmea hukatwa  na majani ya chini yanaweza kuondolewa.

MBOLEA

Mara nyingi katani hua haiitaji sana mbolea kwakua hua na urafiki na mazingira pale inapo pandwa kwenye eneo jipya , lakini inapo pandwa kwenye eneo ambalo limekwishatumika mbolea huitajika , unaweza kutumia UREA, lime ammonium nitrate (LAN) na superphosphate.

UMWAGILIAJI

Kilimo cha katani hakihitaji umwagiliaji kwa kua huhimili ukame japo kua katika kuprocess maji hutumika sana.

UPALILIAJI

Kupalilia ni muhimu sana ndani ya miaka miwili ya mwanzo yaani miaka 2 hadi 3 ni vyema sana kupalilia baada ya kuamishia katika shamba kubwa unaweza kutumia jembe la mkono au hata kemikali, unaweza kuacha magugu kukua wakati wa mvua na ukaya palilia wakati mvua zimeisha

MAGONJWA NA WADUDU WAALIBIFU

WADUDU

  •  Weevil wa katani
  • nguruwe
  • nyani na sokwe

Unaweza kuuwa wadudu kwa kutumia viua dudu ambavyo vimesajiliwa na  kwakulinda shamba ili wanyama kama nyani wasishambulie shamba

MAGONJWA

  • Madoa ya majani
  • kuoza kwa mringoti

Unaweza kuzuia kwa kuweka mbolea ambazo zina calcium na kwa kuweka shamba safi na pia tumia dawa  za kemikali

 

KUVUNA

Kuvunwa kwa mazao inategemea na eneo, kiasi cha mvua udongo na hali ya hewa, lakini kwa kawaida katani huvunwa kwa mara ya kwanza kati ya miaka 3 hadi 4 baada ya kupanda.

Mimea hua na majani 120 hadi 125  ambayo hua na urefu wa 60 cm unatakiwa kuvuna majani ambayo tu yapo tayari .
Majani hua tayari pale rangi inapo badilika kutoka brown iliyo koza hadi kua brown iliyo pauka na majani huvuna kwa interval kwa maana hiyo unaweza kuvuna majani 25 kwa kila mmea kwa mwaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter