Korosho ni mbegu inayokua kwenye mti wa mkorosho. Korosho yenyewe inakua pamoja na tunda linaloitwa bibo na mbegu huonekana nje. Mmea huu ni wa asili ya kaskazini mashariki mwa Brazili. Kati ya mwaka 1560 na 1565 mti huu ulipelekwa hadi Goa, India na mabaharia wa Ureno kutoka hapo ulienea kusini mashariki kwa Asia na mwishoni kufika barani Afrika.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo huenda hufahamu kuhusu korosho
- Korosho hukua kwa mita 10 hadi 15 au futi 32 hadi 50 katika miti ya kijani kibichi inayoitwa mikorosho ambayo ni jamii ya mimea inayotoa maua.
- Mnamo mwaka 2010, Nigeria ilikuwa ni mzalishaji wa juu zaidi wa korosho ambapo ilizalisha takribani tani 650,000.
- Korosho ikiwa ndani ya ganda lake huzungukwa na mafuta yenye sumu ambayo ni sawasawa na asidi iitwayo ‘anacardic’ ambayo inaweza kusababisha muwasho katika ngozi. Korosho hukaangwa au kuchemshwa ili kutolewa katika ganda lake.
- Kutokana na protini iliyopo katika korosho, watu wengine wanaathiriwa na korosho kama wanavyoathiriwa na mimea ya karanga.
- Katika korosho kuna wanga kwa 23% ambayo ni kubwa kuliko karanga zingine.
- Tunda la ukweli la mkorosho ni korosho yenyewe lenye umbo la figo au ghofu ya mabondia ambalo hukua juu ya tunda la bibo ndani ya tunda hili la kweli ndio kuna mbegu moja, korosho.
- Gamba la mbegu ya korosho linaweza kutumika katika matumizi mengi kama vile kilainishi, kuzuia maji (waterproof), rangi nk.
- Bibo la korosho linaweza kuliwa, kupikwa, kuozeshwa na vilevile kutengeneza kilevi.
- Katika baadhi ya maeneo majani na gome la mti wa korosho hutengenezwa kutibu matatizo ya tumbo la kuhara.
- Kabla mbegu ya korosho haijakomaa huwa katika rangi ya kijani kibichi.
- Marekani hutumia zaidi ya 90% ya mazao yote ya korosho ulimwenguni.
- Novemba 23 kila mwaka ni siku ya kitaifa ya korosho.
- Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016, Vietnam inaongoza kwa uzalishaji wa korosho, ikifuatiwa na Nigeria, India, Cote D’ivoire, Philippines, Tanzania, Mali, Guinnea-Bissau, Indonesia na Benin ambayo imeshika nafasi ya kumi.