Home KILIMO Mbinu za kilimo bora

Mbinu za kilimo bora

0 comment 100 views

Kilimo ni sekta ambayo imebadili maisha ya maelfu ya watu hapa nchini. Pamoja na hayo, pia ni sekta muhimu itakayopeleka taifa kwenye uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda hivyo kuna kila sababu kwa wakulima kuzingatia kanuni bora ili kuzalisha kwa tija.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo wakulima wanatakiwa kuzingatia ili kufanya kilimo endelevu na chenye tija:

Kufanya tathmini. Kama wewe ni mkulima mwenye malengo na mipango, unapaswa kupitia hatua hii kwa kuhakikisha wataalamu wa kilimo wanakagua shamba lako ili kujua kama linafaa kwa kilimo cha zao unachotarajia kufanya na vilevile kufahamu historia kamili ya shamba;

Kuwa na ramani. Unapaswa kuchora ramani ya shamba lako. Ramani hiyo inatakiwa kuonyesha maeneo hatarishi kwa mmomonyoko wa udongo, aina za udongo na masuala kama mwinuko mkali n.k.

Mbolea. Hakikisha unaelewa mbolea unazoweka zina virutubisho vya aina gani kabla hujaweka shambani. Ni vyema kununua mbolea kutoka kwenye makampuni yaliyothibitishwa na hakikisha unapewa cheti/risiti inayoonyesha aina na virutubisho.

Viuatilifu vyote viwe vimedhibitishwa na taasisi husika. Aidha, mkulima anapaswa kuwa na mazoea ya kuhifadhi risiti zote za manunuzi. Hakikisha viuatilifu vinahifadhiwa kwa kufuata sheria za nchi na za kimataifa na stoo yako ya madawa ni salama, haishiki moto kwa urahisi, inapitisha mwanga na hewa na vilevile makabati ya kuweka madawa yasiwe yale yanayonyonya maji.

Mkulima anapaswa kutumia viuatilifu ambavyo madhara yake ni madogo kwa viumbe wenye manufaa kama nyuki, viumbe vya majini, wafanyakazi na tabaka la anga (Ozone layer). Pia ni muhimu kufuata ushauri wa wataalamu Mkulima atafute ushauri wa wataalamu kabla ya kunyunyiza dawa. Wakulima na wote wanaohusika kwenye zoezi hili wanatakiwa kupata mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu.

Pamoja na hayo, ni muhimu kwa mkulima kuwa na mpango kazi utakaompatia muongozo sahihi wa namna ya kuanza kilimo chake, kupata mikopo na kuendana na soko. Mpango kazi humfanya mkulima kuendesha kilimo pamoja na biashara yake kisasa zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter