Home KILIMO Mhagama ahamasisha vijana kuwekeza shambani

Mhagama ahamasisha vijana kuwekeza shambani

0 comment 179 views

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama amesema vijana wengi zaidi wakijikita katika sekta ya kilimo, ukuaji wa sekta hiyo utakuwa na hivyo uzalishaji nao utaongezeka. Mhagama amesema hayo alipotembelea mashamba ya wakulima wa majani ya chai kijijini Luangu ambapo kiwanda cha kusindika chai cha Unilever kimejengwa ili kuwainua kiuchumi wakulima wanaofanya kilimo hicho.

Mhagama ameongeza kuwa vijana wapo katika nafasi nzuri ya kuleta mageuzi kwenye kilimo na kubadili maisha yao. Amefafanua kuwa endapo vijana wataamua, mbali na kukuza sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji, pia watapata fursa ya kubadili maisha yao.

Mbali na kutoa wito huo kwa vijana, Waziri Mhagama pia ametoa pongezi kwa kampuni ya NOSC kutokana na jitihada wanazofanya katika kuinua wakulima wadogo wa chai kwa kununua kutoka kwao kupitia ushirika mkoani Njombe. Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa NOSC Filbert Kavia amesema kampuni hiyo inalenga kuwainua wakulima wa chai mkoani humo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter