Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoani Shinyanga Elias Nyanda amesema katika kujiandaa na msimu ujao wa zao la pamba, tayari mizani 600 kati ya 2,000 imeshakaguliwa. Nyanda ameeleza kuwa lengo la ukaguzi huo ni kuondoa udanganyifu ambao wakulima wamekuwa wakifanyiwa. Vilevile, Meneja huyo amesema kuwa kwa kufanya hivyo, wanaongeza tija kwa mkulima kwani wanampa uwezo wa kuzitambua mizani halali pamoja na kuzitumia kwa biashara katika mwaka husika.
Mbali na ukaguzi huo kufanyika mkoani Shnyanga, Nyanda amesema kuwa wamejipanga kutoa elimu kwenye mikoa mingine ambayo imejikita katika kilimo cha pamba kama vile Geita, Mwanza, Mara. Tabora, Simiyu na Kagera.