Home KILIMO TADB, NFRA kuhakikisha mahindi yanapata soko

TADB, NFRA kuhakikisha mahindi yanapata soko

0 comment 109 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine amesema benki hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) wameingia makubaliano ya kuongeza thamani ya mnyororo wa zao la mahindi katika jitihada za kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanapata soko la uhakika na kunufaika na kilimo wanachofanya.

Akizungumza baada ya kikao cha pamoja, Mkurugenzi huyo amesema wamekubaliana kuhakikisha mahindi yanapata soko na kueleza kuwa, kwa msimu uliopita, soko mahindi liliyumba, hivyo makubaliano kati ya taasisi hizo mbili yataleta matumaini kwa wakulima wengi wa mahindi kwa kupata soko la bidhaa hiyo ambayo bei yake ilishuka kutokana na uzalishaji kuwa mkubwa kuliko mahitaji.

“TADB ilishatoa zaidi ya Sh. bilioni 3.4 kwa vikundi 22 vya wakulima katika kufanya kilimo cha kisasa cha zao la mahindi, hivyo kupitia kikao hiki tunawahakikishia wakulima wa mahindi soko la uhakika. Pamoja na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kununua zaidi ya tani 36,000 za mahindi bado shehena nyingi za mahindi zipo kwa wakulima, hivyo kama wadau wa sekta ya kilimo ni wajibu wetu kuhakikisha shehena hizo zinapata soko”. Amesema Justine.

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Vumilia Zikankuba, amesema mazungumzo waliyofanya na TADB yatasaidia kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha zao la mahindi linapata soko.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter