Home KILIMO Unafahamu haya kuhusu Embe?

Unafahamu haya kuhusu Embe?

0 comment 226 views

Msimu wa maembe katika maeneo mengi nchini  huanza  mwezi wa kumi hadi wa kumi na mbili. Tunda hilo ni tunda la kitropiki ambalo hupendwa na watu wengi kutokana na utamu wake na hata virutubisho vilivyopo katika tunda hilo. Hivyo basi hapa chini ntataja mambo kumi ambayo watu wengi hawafahamu kuhusu tunda hilo:

  • Embe ni tunda linalolimwa kwa wingi zaidi katika maeneo yenye joto (tropiki) duniani. Asili ya tunda hilo ni Mashariki mwa India-Burma na Visiwa vya Andaman.
  • Inaelezwa kuwa watawa wa Kibudhi ndio watu wa kwanza kutumia na kusambaza tunda hilo katika maeneoya Malaysiana Mashariki mwa Asia karne ya 5.
  • Kati ya 300 au 400 A.D. mbegu za maembe zilisafirishwa kutoka Asia kwenda Mashariki ya Kati, Afrika Mashariki na hatimaye kwenda Amerika Kusini.
  • Mti wa maembe unaweza kukua hadi mita 35-40 ( sawa na futi 115-130). Inaelezwa kuwa mti wa tunda hili unaweza kuishi hadi miaka 300 huku ukiendelea kuzaa matunda.
  • Tunda hili huchukua kati ya miezi 3-6 kuiva. Pia tunda hili huja katika maumbo, ukubwa na rangi (njano, orenji, nyekundu, na kijani) tofauti tofauti.
  • Maembe yana virutubisho vingi kutokana na kiasi cha ukomavu wake. Kama embe ni la rangi ya kijani basi Vitamin C huwa ya hali ya juu, na ikiwa embe limekomaa ipasavyo basi kiwango cha Vitamin A huwa kikubwa.
  • Inaelezwa kuwa karibia nusu ya uzalishaji wa maembe hufanyika nchini India na kiasi kikubwa cha maembe hutumiwa zaidi na wahindi kuliko kiasi kinachouzwa nje ya India.
  • Embe ni tunda la taifa la India, Pakistan na Ufilipino, pia mti wa tundo hilo ni mti wa Kitaifa nchini Bangladesh.
  • Inaelezwa kuwa, kumpa mtu kikapu cha maembe huchukuliwa kama ishara ya urafiki.
  • Embe linaweza kuliwa kawaida bila kupikwa au linaweza kuchanganywa katika aina mbalimbali ya vyakula. Pia embe linaweza kutayalishwa katika mfumo wa juisi, barafu nk.

Aidha, inashauriwa kupanda miche ya maembe katika msimu wa mvua za mwaka ili miti iweze kupata maji ya kutosha. Mbali na kuendelea kupata elimu kuhusu uzalishaji bora na wa kisasa wa tunda hili,kama mkulima makini ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa miti ya matunda kila baada ya muda ili kuweza kupata mafanikio wakati wa mavuno.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter