Home KILIMO Vijana Tanzania kupatiwa eka 10 kulima

Vijana Tanzania kupatiwa eka 10 kulima

0 comment 166 views

Rais Samia amesema Serikali imetenga hadi eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa za kufanya kilimo nchini Tanzania ili kuiwezesha idadi kubwa ya vijana wenye ari ya kufanya kilimo lakini wakakosa sifa zinazohitajika kwenye taasisi za fedha ili kupewa mikopo kwa ajili ya kilimo.

Sambamba na hilo, Rais Samia ameeleza kuwa hapo baadae vijana hao watamilikishwa eka hizo.
Rais Samia ameyasema haya akijibu swali kuhusu namna ya kuvutia vijana kwenye kilimo, upatikanaji wa ardhi, teknolojia na fedha wakati wa ufunguzi wa mkutano unaohusu Kilimo huko Dakar nchini Senegal na kusisitiza kuwa Tanzania iko katika mchakato wa kupokea maombi kwa kundi la kwanza la vijana watakaopata fursa ya kupata mafunzo ya miezi mitatu kuanzia katikati ya mwezi Februari.

Pamoja na Serikali kujizatiti, Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imetangaza kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 120 kwa ajili ya sekta ya kilimo ikiwemo umwagiliaji na kujenga kituo cha usafirishaji na usambazaji mbolea kwenye mpango huo unaowalenga vijana na wanawake ujulikanao kwa jina la BBT, ‘Ujenzi wa Kesho Bora’.
Tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa BBT miezi sita iliyopita tayari Tanzania imeweza kutenga jumla ya eka 600,000 kwa nchi nzima ambapo pia tayari shughuli ya kusafisha mashamba hayo imeanza.

Soma: Sekta ya kilimo kukua kwa 10% 2030: Rais Samia

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter