Home KILIMO Wakulima walia tozo kulipwa kwa dola

Wakulima walia tozo kulipwa kwa dola

0 comment 99 views

Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA), kimetoa malalamiko kwa Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga kuhusu suala la kulipa tozo za ungizaji wa pembejeo na viuatilifu kwa dola badala ya shilingi. Mwenyekiti wa TFA, Peter Sirikwa amesema kutokana na kulipa kwa dola tozo za uingizaji wa pembejeo na viuatilifu nchini, bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa kwa gharama kubwa kwa wakulima, hivyo kueleza kuwa kama mabadiliko yatafanyika itasaidia bei za pembejeo kuacha kubadilika mara kwa mara.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameomba wapewe mashamba kwa ajili ya madarasa katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe na Mbeya ili waweze kujishughulisha zaidi na kilimo cha kisasa na kutoa elimu kwa wakulima.

Kwa upande wake, Waziri Hasunga amesema kuwa serikali pamoja na wadau wa kilimo wanashirikiana katika uwekezaji wa viwanda vya pembejeo nchini. Lengo ni kuona mbolea inazalishwa nchini. Ametoa wito kwa chama hicho kufikiria kuwekeza katika kiwanda cha pembejeo ili kupunguza uagizaji wa pembejeo nje ya nchi na kufanya gharama kuwa ya nafuu kwa wakulima.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter