Home KILIMO Wakulima wasisitizwa ubora

Wakulima wasisitizwa ubora

0 comment 100 views

Katibu Tawala wa mkoani Songwe, Vanscar Kulanga ametoa wito kwa wakulima wa zao la alizeti kubadilika na kufanya kilimo chao kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora yaani matumizi ya mbegu bora ili waweze kuongeza mavuno. Katibu huyo ameeleza hayo alipokuwa kifungua kongamano la wadau wa kilimo cha alizeti lililofanyika mkoani Mbeya chini ya Programu ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo hapa nchini (AMDT).

“Ni wajibu wetu serikali kwa kushirikiana na wadau kama Programu ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT) katika kuhakikisha wakulima wetu wanapewa elimu na pembejeo stahiki itakayowawezesha kufanya kilimo cha alizeti kuwa chenye manufaa kwao binafsi na pia kwa taifa”. Amesema Kulanga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AMDT nchini, Michael Kairumba lengo kubwa la programu hiyo ji kumuwezesha mkulima kupata elimu pamoja na masoko ya uhakika kwa kumuunganisha na mtandao wa watoa huduma za msingi kama taasisi za pembejeo, taasisi za fedha na taasisi zinazoshughulika na masuala ya bima. Pamoja na hayo, ametoa wito kwa wakulima wa alizeti kulima kwa wingi kwa kuwa soko ni kubwa ndani na nje ya nchi.

“Tunakusudia kumfanya mkulima kuwa na nguvu katika mnyororo wa thamani wa zao la alizeti maana kwa muda mrefu amekuwa ni mnyonge na asiyekuwa na maamuzi katika masoko tunataka kupitia mbinu bora anazofundishwa aweze kuinuka kiuchumi ili nae awe na maamuzi katika soko”. Amesema Mkurugenzi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter