Home KILIMO Waziri Mkuu ataka tathmini ya Zao la Korosho

Waziri Mkuu ataka tathmini ya Zao la Korosho

0 comment 99 views
Na Mwandishi wetu

Baada ya kufanya mazungumzo na wadau wa zao la korosho ofisini kwake mjini Dodoma, Waziri Mkuu ameagiza kufanyika kwa tathmini ya zao la korosho na kutaka Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Korosho kutoa tathmini ya maandalizi ya msimu ujao katika maeneo ya mashamba, miche, viatilifu na pembejeo.

Majaliwa amesema serikali haijapata nafasi na kukaa pamoja na wadau wote tangu kuamua kusimamia mazao makuu matano yaani pamba, chai, kahawa, tumbaku na korosho. Ameongeza kuwa serikali imeamua kufuatilia usimamizi wa mashamba kwa kusimamia upatikanaji wa mbegu, miche na pembejeo. Pia itafuatilia uvunaji na mfumo mzima wa masoko ya korosho pamoja na mifumo ya ushirika katika baadhi ya mazao.

Waziri Mkuu amewaambia wadau waliokuwepo katika mazungumzo hayo kuwa, kuna tatizo la tathmini ya maandalizi ya msimu kutotekelezwa kwa wakati hivyo Bodi kwa kushirikiana na Wizara husika zote zinapaswa kufanya hivyo kwa msimu ujao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter