Home KILIMO YARA yaendelea kuhamasisha kilimo bora

YARA yaendelea kuhamasisha kilimo bora

0 comment 283 views

Bwana Shamba Mkuu wa YARA Tanzania, Peter Assey amesema kampuni hiyo inaendelea kutoa elimu na maarifa ya kilimo bora hususani katika elimu ya afya na udongo kwa wakulima wa mikoa ya nyanda za juu kusini. Akizungumza kufuatia utiaji saini makubaliano ya kuinua kilimo kati ya kampuni hiyo, TADB na TARI, Assey amesema makubaliano hayo yanalenga kumuinua mkulima na hivyo kuchochea uzalishaji.

“Hii ni hatua nyingine muhimu kwa maendeleo ya mkulima hapa nchini kwa kuwa makubaliano haya yataleta tija kubwa kwa taifa kwa kuwa yatakomboa wakulima wengi kwa kukuza kipato chao. Lakini jambo la muhimu zaidi ni kufikia azma ya serikali ya kuifanya Tanzania iwe na uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025”. Amesema Bwana Shamba huyo.

Pamoja na hayo, Assey ameongeza kuwa, kwa kushirikiana na TARI na TADB, taasisi hizo tatu zimejipanga kutoa elimu ya udongo kwa wakulima ili kuchochea uzalishaji wenye tija na hivyo kukuza kipato cha wakulima.

“YARA tumekuwa tukipima udongo kabla ya kugawa mbolea, lakini tumegundua kiwango cha tindikali kipo chini sana hasa katika maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Hivyo kwa kushirikiana na TARI tutatoa elimu juu ya matumizi ya chokaa ambayo huongeza kiwango cha tindikali kwa kutumia wataalamu wa ndani ili kuboresha uzalishaji”. Ameeleza Assey.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter