Home KILIMO Zoezi uhakiki wa mashamba lapamba moto

Zoezi uhakiki wa mashamba lapamba moto

0 comment 139 views

Zoezi la uhakiki na upimaji wa mashamba kwa ajili programu ya Building a Better Tomorrow (BBT ) linaenda vizuri kutokana na ushirikiano na utayari unaooneshwa na viongozi na wananchi wa mikoa ya Kigoma na Kagera.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Mhandisi Juma Mdeke.

Mhandisi Mdeke amesema anatambua na kupongeza ushirikiano wanaoupata kutoka kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji katika uendeshaji wa zoezi hilo.
Kwa upande wake kiongozi wa timu ya wataalam inayohakiki na kupima mashamba kwa ajili ya programu ya BBT mkoani Kagera Mhandisi Godwin Makori ameeleza kuridhishwa kwake na ushirikiano na utayari unaooneshwa na viongozi wa Mkoa wa Kagera kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri hadi Vijiji.

“Kazi inaenda vizuri, tunapata ushirikiano kwa viongozi wa ngazi zote jambo linalopelekea kufanya kazi tuliyoagizwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa usahihi,” ameeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbale Kata ya Kitobo Wilaya ya Misenyi Frolian Lwiza amesema viongozi wa kijiji na vijana wa kijiji hicho wanausubiri kwa hamu programu ya BBT.
Mwenyekiti Lwiza ameongeza kuwa wananchi wa kijiji cha Mbale wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwani shamba hilo lilitengwa wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya uzalishaji wa chakula hivyo uendelezaji wa eneo hilo ni kumuenzi Mwalimu Nyerere.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter