187
Katika jitihada za kuunga mkono Serikali kuboresha sekta ya afya, Benki ya stanbic imetoa kadi 200 za bima ya afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo, akimkabidhi mtoto Bless John, mmoja kati ya watoto 200 wanaoishi katika mazingira magumu walionufaika na bima ya afya kwaajili ya kupata matibabu kutoka benki ya Stanbic Tanzania jijini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Standard Bank kanda ya Afrika, Tshepo Dlamini Ramoshaba na Afisa Ustawi wa Jamii, Asia Jingu (kushoto).