Katika jitihada za kuhamasisha tabia ya kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha afya, kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom imedhamini wanafunzi 51 kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini Dodoma pamoja na wafanyakazi wake 35 katika mbio za Capital City Marathon jijini dodoma mwishoni mwa wiki.
Miongoni wa washiriki alikua ni Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Kati, Bi Grace Chambua.

Mkuu wa mauzo wa kanda ya kati wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Grace Chambua (wa nne kutoka kulia mwenye kofia) akijiandaa kuanza mbio za Marathon za Capital City zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma, kampuni hiyo ilidhamini wanafunzi 51 kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko jijini humo pamoja na wafanyakazi wake 35 ili kuwajengea tabia ya kufanya mazoezi na kuboresha afya zao.