Shirika la ndege la AirFrance limezindua safari zake za moja kwa moja kutoka Paris nchini Ufaransa hadi Dar es Salaam nchini Tanzania.
Mapokezi ya ndege hiyo aina ya Boeing 787-9 yamefanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Juni 12, 2023.
Uzinduzi wa safari hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Fatma Rajab.
Serikali imesema safari hizo zinalenga kuimarisha ushirikiano wa utalii na biashara kati ya Tanzania na Ufaransa.
Toka mwaka 2021, Air France inafanya safari zake kutoka Paris hadi Zanzibar mara mbili (2) kwa wiki na sasa imeamua kufanya safari za moja kwa moja kutoka Paris hadi Dar es Salaam kupitia Zanzibar mara tatu (3) kwa wiki.
Kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Air France kutokea Dar es Salaam kwenda Paris kutafanya idadi ya Mashirika ya Ndege ya yanayofanya safari za Kimataifa kutokea JNIA kufikia ishirini na mbili (22).