Home Lifestyle Unatamani kua mfano wa kuigwa(ROLE MODEL) katika jamii yako

Unatamani kua mfano wa kuigwa(ROLE MODEL) katika jamii yako

0 comment 162 views

Mtu wa mfano(Role model) ni mtu ambaye,huwa anaangaliwa kama mfano pale watu mwengine wanapotaka kufanya majukumu fulani;iwe ya uwanafunzi, urafiki, ujirani, kazini, au sanaa na hata michezo.

Yawezekana kila mmoja wetu ana mtu wake anayemuangalia kama mtu wake wa mfano.

Hasa mtu anapokuwa katika rika la kuanza kujitambua, mara nyingi huanza kwanza kuvutiwa na sifa za watu wengine anaowaona kila siku.Na ndio maana,unatakiwa kuwa makini sana mtoto wako kipindi cha ukuaji,anachangamana au kuwaangalia watu wa aina gani.

Kwa mtoto,haitajalisha huyo mtu aliyevutiwa naye anafanya jambo jema au baya.Kama amevutiwa jinsi anavyofanya na yeye atataka kuwa kama huyo mtu kwa kufuata njia zake.

Unapobahatika kuvutiwa na mtu, na ukamchagua kuwa mtu wako wa mfano, anaweza kuwa chanzo cha wewe kufikia mafanikio fulani unayotamani kuwa nayo.

Ikiwa mtu wako wa mfano yuko karibu na mazingira yako unaweza ukafanya hili:

1.TAFUTA NAFASI YA KUZUNGUMZA NAYE

Hii ni hatua ya kwanza,unaweza kuitumia kumfahamu mtu wako wa mfano kiundani njia alizopitia kuwa hapo alipo.Usifiche hisia zako kumueleza jinsi gani unavutiwa na tabia yake na ungependa kuwa kama yeye.Hiyo itamfanya ajisikie vizuri,na akupe ushirikiano, kwa kuwa kila binadamu anapenda awe anavutia wengine.

      *USIMUULIZE MASWALI MAGUMU

Unapopata nafasi,ya kuzungumza na mtu wako wa mfano haina maana kwamba, amekuamini vya kutosha kukuelezea kila kitu kuhusu njia alizopitia.Ila,kuwa na maswali mepesi ambayo yatamfanya yeye wakati anakuelezea aguse eneo ambalo wewe haungeweza kumuuliza kwa urahisi.

Hata kama haujakutana naye uso kwa uso lakini umeweza kuwasiliana naye kwa njia nyingine za kieletroniki,kuwa makini katika kuuliza maswali.

      *JENGA SHAUKU

Njia yoyote ya kujifunza jambo,kwa ufanisi ni kuweka shauku ya kutaka kujua zaidi,wakati unazungumza naye hata kama kuna kipengele unaona hakija kuvutia tengeneza shauku ili upate kujifunza zaidi kutoka kwake.

Yafuatayo ndio unapaswa kufanya baada ya kuchagua mtu wako wa mfano:

  • IGA MEMA ANAYOFANYA/ALIYOFANYA

Usitarajie kwamba,kila tendo analotenda mtu wako wa mfano ukilifanya wewe pia litakuwa jema.

Yawezekana mtu wako wa mfano umesoma njia zake alizopitia kupitia maandishi na wala sio kutoka mdomoni mwake,unapaswa utambue jamii zinatofauti ya kutafsiri matendo.

Kama ni rafiki kwa kila mtu,na wewe kuwa hivyo, kama ni mtu wa kutabasamu, nawe fanya hivyo, na kama anasaidia watu na wewe usisite kufanya hivyo pale unapokuwa na uwezo huo.

  • SOMA WASIFU WAKE MARA KWA MARA

Unapokuwa na tabia ya kusoma wasifu wa mtu wako wa mfano,itakusaidia kufahamu kwa nini aliweza kufanya anachofanya sasa.

TAFUTA MTU WAKE WA MFANO ALIKUWA NANI

Hii itakusaidia, kujua kuwa yeye aliweza kiasi gani kufanikiwa kupitia mtu wake huyo wa mfano na tofauti yao iko wapi.

Kila mmoja wetu anaweza kuwa mtu wa mfano katika jamii yake kwa kufanya yafuatayo:

 

JITAMBUE

Ukitaka kuwa mtu wa mfano,katika jamii yako ni lazima kwanza uwe wewe umejitambua.Unataka kuwa nani na kwa nini.

Hii itakupelekea ufanikiwe katika yule unayetamani kuwa.Hii itawafanya wanaokuangalia wapate shauku ya kutaka kujifunza zaidi kupitia wewe.

KUWA NA MSIMAMO

Kama umechagua kufanya jambo fulani,na jamii ikajua wazi kwamba wewe unafanya hilo jambo usiwe kigeu geu. Utawachanganya watu wasijue unataka nini hasa.Kama ulichagua siasa na ukakutana na ugumu endelea kupambana mpaka upate suluhisho sio ugumu kidogo tu ushabadilisha msimamo.Hakuna mtu atakaye tamani kuwa na mtu wa mfano asiyejielewa.

ISHI NDOTO ZAKO

Kama ulitamani siku moja ukipata kitu fulani ndio roho yako itafurahia,ukipata huo uwezo usisite kufanya hilo.Kwani utawafanya watu wengine waone wewe ni mfanikishaji ndoto hivyo unapaswa kuigwa.

SAIDIA WATU WENGINE

Chagua kuwa mtu mzuri,na wa msaaada kwa watu wengine.Wapokee wengine maishani mwako.Ukipokea watu vile walivyo utawafanya wajione wana thamani mbele yako nao pia watatamani kuwa kama wewe

TIMIZA MAJUKUMU YAKO

Kama ni mzazi,fanya mazungumzo na watoto wako na kufuatilia maendeleo yake/yao ya kila siku na pia majukumu mengine ya familia itawafanya watoto wako wasiende nje kutafuta watu wengine wa mfano bali utakuwa wewe mzazi wao ndio mtu wao wanayetamani kuwa.Kwani hulka ya binadamu siku zote ni kuwa shujaa.

 

HEBU TUANZE LEO KUWA AINA YA WATU AMBAO WENGINE WANAWEZA KUIGA YALE TUNAYOYAFANYA.

USIKUBALI KUIACHA DUNIA HII HUKU WATU WAKISHUKURU KUONDOKA KWAKO.

Special thanks and credits goes to; JANE ORGENES NG’ENI.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter