Home Uncategorized Athari za kutumia mtandao kupita kiasi

Athari za kutumia mtandao kupita kiasi

0 comment 117 views

Kadri muda unavyozidi kwenda maboresho ya teknolojia za mawasiliano na upatikanaji wa nyaraka zimeendelea kuboreshwa zaidi. Mtandao wa intaneti umerahisisha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa na mawasiliano duniani kote. Waru wengi wanategemea mtandao kufanya mambo mbalimbali lakini kama inavyoeleweka, kila kitu chenye faida siku zote huwa hakikosi kasoro.

Zifuatazo ni hasara zinazotokana na matumizi ya intaneti yaliyopitiliza:

Kupoteza muda

Watu wengi hujikuta wanatumia muda mwingi kwenye mtandao badala ya kufanya vitu vya muhimu. Asilimia kubwa ya vijana hutumia muda mwingi kuperuzi katika intaneti na mitandao ya kijamii kama vile Instagram, badala ya kufanya kazi au masuala yanayoweza kuwaingizia kipato au kuwanufaisha.

Taarifa za uongo

Ni rahisi kuweka taarifa au nyaraka za uongo mtandaoni na mabilioni ya watu kuweza kuona taarifa hizo na kuzipokea kwa namna tofauti. Taarifa hizi huleta athari mbalimbali kama kumharibia mtu heshima katika jamii hivyo ni muhimu kuwa makini na taarifa zinazopatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na kuwa makini na chanzo cha habari.

Biashara haramu

Si kila mtu huwa na nia njema kila wakati, hivyo hata kama intaneti ni msaada mkubwa katika maisha ya kila siku, watu wametumia fursa hiyo kujihusisha na biashara haramu. Biashara hizo ni kama uuzaji wa silaha, madawa ya kulevya nk. Inashauriwa kuwa makini na programu unazojihusisha nazo mtandaoni ili kuepuka masuala haramu.

Matumizi mabaya ya fedha

Intaneti si teknolojia ya bure, ili kuweza kuitumia unapaswa kuwa na kifaa cha kielektroniki kama simu na vilevile unalazimika kuweka fedha ili kupata huduma. Matumizi makubwa ya intaneti hupelekea matumizi makubwa ya fedha, jambo ambalo linaweza kuwa ni tatizo hasa kama unatumia fedha nje ya bajeti yako.

 

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter