Home Uncategorized Fahamu haya kuhusu mtandao wa 5G

Fahamu haya kuhusu mtandao wa 5G

0 comment 126 views

Kupitia simu za mkononi, watu hufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupakua na kutuma picha na video, kuangalia mitandao ya kijamii na kuangalia machapisho mbalimbali nk. Wakati hayo yote yanafanyika watu huwa hawafurahii kusubiri kwa mfano wakati wa kupakua video watu hufurahia mchakato huu ukifanyika kwa haraka zaidi na ndio maana teknolojia mpya zinaendelea kuanzishwa kila siku.

Hivyo basi yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kujua kuhusu mtandao mpya wa intaneti wa 5G:

  • 5G ni muendelezo wa mtandao wa intaneti kutoka 4G. Mtandao huo umelenga kuongeza kasi ya kupakua hadi GB 10 kwa sekunde. Hiyo inamaanisha kuwa filamu nzima inaweza kupakuliwa ndani ya sekunde chache tu.
  • Kutokana na kasi kubwa, mtumiaji wa 5G ana uwezo wa kuunganisha vifaa vingi kwa wakati mmoja.
  • Ikiwa unaona unatumia fedha nyingi katika malipo ya 4G, basi tambua kuwa katika mtandao wa 5G mambo yatarahisishwa katika kasi lakini malipo lazima yataongezeka ikiwa ni pamoja na kununua simu zinazokubali mtandao huo.
  • 5G inategemea kuzinduliwa mwakani duniani kote.
  • Teknolojia hiyo itarahisisha zaidi shughuli zinazotumia mtandao huo kufanya kazi. Kwa mfano kwa nchi za nje shughuli moja wapo ni uendeshaji wa vyombo vya usafiri.
  • Tayari makampuni mbalimbali ya simu yameshaanza kutengeneza vifaa vya kielektroniki ambavyo vinaendana na mfumo huo.

Teknolojia zinazinduliwa na kuboreshwa lakini hiyo haimaanishi kuwa kila teknolojia inayozinduliwa lazima kila mtu awe nayo. Kuna umuhimu mkubwa wa kutathmini na kuangalia kama zina manufaa katika kazi na maisha yetu ili kuepuka kutumia fedha nyingi.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter