Kampuni ya Motorola imezindua simu mpya ya Motorola One Macro hapo jana nchini India. Moja ya sifa kubwa ya simu hiyo ni uwezo wake wa kupiga picha vitu vidogo ambavyo katika hali ya kawaida huonekana vidogo zaidi lakini kupitia moja wapo ya kamera ya nyuma yenye Megapixel 2 vitu hivyo huonekana vikubwa katika picha, jambo ambalo linaweza kuwafurahisha watu wanaopendelea kupiga picha vitu vidogo kwamfano wadudu.
Simu hiyo itaanza kupatikana katika soko la mtandaoni la Flipkart kuanzia tarehe 12 mwezi huu kwa gharama ya India INR 9,999 ambayo ni sawa na Shilingi 323,448.98 za Kitanzania kwa sasa.
Pia simu hiyo imezinduliwa katika rangi moja tu ambayo ni –Space blue. Hivyo basi zifuatazo ni sifa za simu hiyo:
- Kioo : ukubwa wa kioo cha simu hiyo ni inchi 6.21 chenye IPS LCD capacitive touchscreen, ambacho kina uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16.
- Mfumo wa uendeshaji: Android 9.0 (Pie)
- Chipset: Mediatek MT6771 Helio P70 (12nm)
- Uwezo wa processor (CPU): Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53)
- Uwezo wa GPU: Mali-G72 MP3
- Ukubwa wa RAM: ni 4GB
- Ukubwa wa ndani : ni GB64 lakini unaweza kuongezwa kwa memory card yenye uwezo hadi wa GB 512.
- Kamera ya mbele ina : Megapixels 8 ambayo ni HDR, katika upande wa video ina uwezo wa kuchukua video hadi za 1080p@30fps.
- Kamera za nyuma ziko tatu: kamera moja wapo ina Megapixel 13, huku kamera nyingine ikiwa na megapixel 2 (hii ni kwaajili ya picha za macro), na kamera ya tatu ina Megapixel 2 (hii ni kwaajili ya picha za Potrait). Pia katika kamera ya nyuma kuna LED flash, HDR, panorama na katika upande wa video ina uwezo wa kuchukua video hadi 1080p@30/60/120fps.
- Betri : katika simu hii kuna betri isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh. Motorola imeeleza kuwa chaji katika simu hiyo inaweza kukaa hadi siku mbili ikiwa mtumiaji atatumia kwa matumizi ya kawaida.
Aidha, simu hii ina sensor ya Fingerprint (kwa nyuma), ina Redio FM, inatumia line mbili ambazo ziko katika mfumo wa Hybrid Dual Dual SIM (Nano-SIM, Dual stand-by). Pia simu hii ina uwezo wa mtandao wa 2G, 3G, na 4G.