Home VIWANDANISHATI Dk. Kalemani akerwa umeme kukatika mara kwa mara

Dk. Kalemani akerwa umeme kukatika mara kwa mara

0 comment 43 views

Kufuatia matukio ya umeme kukatika mara kwa mara nchi nzima, Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuwavua nyadhifa manaibu wakurugenzi kutoka sekta ya uzalishaji na usambazaji wa Shirika la umeme nchini (TANESCO) kufuatia uzembe uliojitokeza kwenye gridi ya taifa, hali iliyopelekea kukosekana kwa umeme.

Akizungumza baada ya kukutana kwa dharura na Bodi ya TANESCO, Dk. Kalemani amesema katika kipindi cha miezi miwili, gridi ya taifa imetoka mara nne kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 14, 2018 na kudai kitendo hicho ni hatari kwa usalama ikizingatiwa kuwa nchi ina ziada ya umeme wa wastani wa megawati 252.

“Lazima kuchukua hatua kuhakikisha hilo halijitokezi. Mwenyekiti (wa bodi) unda timu mahsusi kuanzia leo ya kuchunguza na kufuatilia jambo hilo kwa kushirikisha tasnia na taasisi mbalimbali si TANESCO pekee. Ndani ya siku saba nipate matokeo ya nini chanzo cha tatizo hilo ili lisijirudie kabisa. Jambo hili linapotokea ina maana kuna uzembe katika usimamizi ama kutofuatilia maagizo ya serikali”. Amesema Waziri Kalemani.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter