Home Uncategorized Vijana BBT waonesha utayari wa kujifunza zaidi

Vijana BBT waonesha utayari wa kujifunza zaidi

0 comment 156 views

Vijana waliopo katika Mradi wa Kujenga Bora ya Kesho (Build Better Tomorrow BBT) wameonesha utayari wa kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo na biashara ili kupata ujuzi na elimu ya kujiajiri wenyewe.

Mratibu wa BBT Vumilia Zikankuba ameeleza hayo wakati anajibu swali la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango kuhusu utayari walionao vijana hao ili Serikali izidi kuongeza kasi katika kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa za kilimo biashara.

Mmoja wa wanufaika wa programu hiyo Fatma Kandoro amesema miongoni mwa maarifa muhimu waliyopewa ni kutambua na kutumia mbegu zilizothibitishwa kitafiti ili kupata matokeo mazuri kwenye mavuno.

Kandoro ambaye ana elimu ngazi ya shahada ya uzamili ya Menejment ya Rasilimaliwatu amesema vijana wanatakiwa kuondokana na fikra potovu kuwa kilimo ni shughuli ya watu waliokosa elimu au waliokosa shughuli ya kufanya.

Ameongeza kuwa maarifa aliyoyapata kwenye kituo atamizi cha MAT Uyole, kwa sasa yupo tayari kujiajiri na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengine.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter