Home Uncategorized Vodacom yaandaa futari kwa wateja wake

Vodacom yaandaa futari kwa wateja wake

0 comment 142 views

Kampuni ya simu ya Vodacom imeandaa hafla ya futari kwa wateja wake katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamis Kigwangalla, Sheikh Othman Zuberi kutoka BAKWATA na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Pia miongoni mwa wageni waalikwa walikua wafanyakazi na wateja mbalimbali wa Vodacom Tanzania.

Wageni hao walialikwa na mwenyeji wao Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Hisham Hendi. Waislam duniani kote wanatazamia kumaliza mfungo wa Ramadhan siku ya Jumatano tarehe 5 Juni ambapo kutakua na sherehe za Eid kuhitimisha mfungo huo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh Hamis Kigwangalla akisalimiana na Sheikh Othman Zuberi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kitengo cha Biashara cha kampuni ya Vodacom Tanzania kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Arjun Dhilon.

Waziri wa maliasili na utalii, Mh Hamis Kigwangalla (Katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi (Kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Idara ya biashara ya kampuni hiyo katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja wateja wake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh Hamis Kigwangalla akipakua chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na kitengo cha Biashara cha kampuni ya Vodacom Tanzania kuadhimisha mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na wateja wake hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Wageni waalikwa pamoja na wateja wa Vodacom katika hafla ya futari.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter