Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Makamu wa Rais atetea wanawake wajasiriamali

Makamu wa Rais atetea wanawake wajasiriamali

0 comment 41 views
Na Mwandishi wetu

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema inashangaza kuona riba inakuwa kubwa kwenye mikopo wakati ikiwa ndogo kwenye amana riba, hali iliyopelekea atoe agizo kwa taasisi za kifedha pamoja na benki kuwa na masharti mepesi maalum kwaajili ya wanawake ambao ni wajasiriamali wadogo.

Samia ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji la Wanawake la Dar es salaam ambapo mbali ya kuagiza taasisi hizo kurahisisha mifumo ya mikopo kwa wanawake, amewataka wanawake kutumia fursa zilizopo na kujikwamua kiuchumi badala ya kupoteza muda wao na mambo yasiyo na tija.

Naye Mwenyekiti wa jukwaa hilo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema wanawake ndio watakaolikomboa taifa letu na umaskini hivyo hadi kufikia mwaka 2020, ameshauri wanawake kuwezeshwa ili wapate fursa ya kushirika katika Tanzania ya viwanda.

Wakati huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC) Jacqueline Maleko amesema mpaka hivi sasa chama hicho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea kuweza kusaidia wanawake wajasiriamali mipakani,

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter