Home FEDHA YAFAHAMU MASWALI AMBAYO UNAPASWA UJIULIZE KABLA HUJAFANYA SHUGHULI YOYOTE

YAFAHAMU MASWALI AMBAYO UNAPASWA UJIULIZE KABLA HUJAFANYA SHUGHULI YOYOTE

0 comment 127 views

1.NINI FAHARI KATIKA MAISHA YANGU?

Ukiwa mtu wa kufuata moyo wako katika kufanya vitu vyako, watu hawatakuwa wanakubaliana na wewe mara kwa mara.
Unapofanikiwa kupata kitu kinachokupa furaha, si kila mtu atakuwa anafurahi kwa ulichogundua.
Ukiwa mkarimu na mnyenyekevu kwa watu bado kuna wengine watakaohoji kwanini unafanya hayo.
Unapokuwa muaminifu kwa watu kuna watu watakaoutumia uaminifu wako kutaka kukuzima.
Ukiamua kuwa msaada kwa watu kuna watu watakaotaka kuutumia msaada huo kukurudisha chini.
Lakini usiruhusu yeyote kati ya watu hawa wakurudishe nyuma kufanya jambo ambalo wewe linakupa fahari na furaha katika maisha yako.
Unachopaswa kujua ni kuwa mwisho wa siku unachopaswa kuangalia ni wewe na furaha yako na si wao.
Itakapofikia wakati ukajiuliza swali, “je, nina fahari na jinsi ninavyoishi?” Jibu liwe ndio.
2.JE, NINALETA MABADILIKO CHANYA KATIKA MAISHA?
Hata kama kuna hali ya kukatisha tamaa, jitahidi kufanya jambo sahihi kila siku.Kila siku ishi kwa kufuata nguvu ya upendo na ukweli.Kwani kila siku ukweli na upendo ndio huchomoza juu zaidi.Endelea kuingiza mazuri yako ulimwenguni, kila unapopata nafasi hata kwa jambo dogo.
Ni katika mkusanyiko wa matendo ya vitu vidogo vidogo ndio vinaleta mabadiliko ulimwenguni.
Unaweza ukawa huoni ni kwa jinsi gani matendo yako mema yanavyoleta mabadiliko kwa sasa lakini muda utakapofika utashuudiwa tu na watu.
3.KITU GANI NATAMANI KUWA NACHO, NA KWA NINI?
Ukishajua jibu la hili swali, jikumbushe kila siku katika maisha yako.
Unatakiwa uchambue, bila shaka yoyote, sababu mahsusi kwanini unafanya shughuli unayofanya.
Mafanikio hutokea pale tu ambapo kuna lengo mahsusi na sababu ya kinachofanywa na mtu husika.
Unapokuwa na sababu ya kufanya shughuli fulani unakuwa na lengo kuu nyuma ya nguvu zako unazowekeza.
Unapoweza kuunganisha sababu na matarajio ya unachotaka upate, utaweza kutengeneza nidhamu na uvumilivu kwa kile unachofanya katika shughuli yako.
Jipe mwenyewe sababu za msingi ili uweze kuyafikia mafanikio kwa nguvu zote.
4.VITU GANI NI VIZUIZI KWANGU?
Kufahamu kizuizi chako, ni njia ya kutambua namna ya kukabiliana nacho.Kizuizi siku zote huendelea kuwa kizuizi kama  haujakitambua.Na endapo unatokea kukitambua kizuizi chako kinakuwa ni changamoto tu.
Angalia katika mazingira yako na bainisha vitu gani ni changamoto kwako halafu vitumie kufungua fursa za maendeleo katika maisha yako.
Ukiweza kuvibainisha vyote utakuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa kwasababu unajua ulipo, wapi unataka kwenda na una nyenzo gani kufanikisha unachotaka.
Kumbuka njia yenye vikwazo ndio siku zote humpeleka mtu kilele cha juu kabisa.
Na kikubwa si kukwepa vikwazo, bali ni kukabiliana navyo mpaka mwisho.
5.MPANGO WANGU MBADALA NI UPI?
Ni wazi kuwa kila mmoja wetu hukosea katika jambo fulani anapolifanya, lakini unachopaswa kufikiria ni vipi utaweza kuibuka na njia mbadala kutatua tatizo lako.
Anza kuchukua hatua mpya mara unapoona hatua za mwanzo zimeshindikana.
Si lazima uanze na hatua kubwa ili ufike haraka, la, unaweza kuanza na hatua ndogo ndogo ambazo zitakuwa zinakupa nafasi ya kutafakari namna ya kuongeza kasi.
Fanya unalotamani kufanya kwa kutumia rasilimali ulizonazo sasa.
JIJENGEE TABIA YA KUJIULIZA MASWALI KWA KILA JAMBO UNALOFANYA ILI KUJUA KAMA UTAWEZA KUFANIKISHA AU LA.
 
UKIWEZA KUJIULIZA MASWALI YA HAPO JUU NA ZAIDI UTAJITENGENEZEA NAFASI YA KUSHINDA KILA UNACHOFANYA.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter