Home VIWANDAMIUNDOMBINU Bandari ya Bagamoyo kuendelezwa

Bandari ya Bagamoyo kuendelezwa

0 comment 98 views

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko amesema mamlaka hiyo na serikali kwa ujumla inaendelea kujadiliana na wawekezaji wa bandari mpya ya Mbegani-Bagamoyo ili kuangalia mfumo bora zaidi wa kuipatia serikali mapato.

Kakoko ameeleza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu na mara baada ya ujenzi kukamilika, itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena zinazowasili nchini na zinazoenda nchi jirani za Burundi, Congo, Malawi, Rwanda, Uganda pamoja na Zambia.

“Mwaka 2009 TPA ilimwajiri Mtaalam Mwelekezi (M/s Hamburg Port Consulting GmbH) ambaye alifanya upembuzi yakinifu ambao pamoja na mambo mengine, alionyesha kwamba mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani-Bagamoyo ni wenye manufaa kiufundi, kifedha, kiuchumi na kijamii”. Amedai Kakoko.

Mkurugenzi huyo pia amesema gharama za ujenzi wa bandari inakadiriwa kufikia Dola za Marekani 1.2 bilioni ambapo, serikali imeamua kutekeleza mradi huo kwa kushirikisha sekta binafsi kutokana na ukubwa wa gharama.

“Serikali ya China imeonyesha nia ya kushiriki katika kuendeleza mradi huu na kuiteua kampuni ya China Merchants Holdings International Limited (CMHI) kushiriki katika majadiliano husika… Wakati majadiliano yanaendelea, CMHI alipendekeza kumjumuisha Serikali ya Oman kupitia taasisi yake ya State General Reserve Fund (SGRF) kuingia katika ubia huu. Vipengele vya mikataba ya mradi baina ya serikali na wawekezaji vilishasainiwa Oktoba, 2015 na majidiliano yanaendelea”. Amefafanua Kakoko.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter