Home VIWANDAMIUNDOMBINU Changamoto ya maji Chalinze kujadiliwa

Changamoto ya maji Chalinze kujadiliwa

0 comment 138 views

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo kuitisha mkutano na wadau wote wanaohusika na mradi wa maji Chalinze Januari 29, ili kujadili changamoto za upatikanaji wa maji katika Halmashauri hiyo. Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo katika eneo la Chalinze, Aweso amesema mpaka sasa mradi huo umefika asilimia 78 na kueleza kuwa, ameona changamoto katika uendeshaji wa mradi huo ikiwemo kuwepo kwa vituo vya maji zaidi ya 200 lakini 86 pekee ndio vinafanya kazi, na vilevile changamoto ya uendeshaji.

Naibu Waziri huyo amewataka Watendaji kutoka Wizara ya Maji kuhakikisha wanatafuta wakandarasi wenye weledi na kazi zao ili kuhakikisha miradi inasimamiwa ipasavyo bila kusuasua.

“Mkandarasi anayesimamia mradi huu ni changomoto, hatuwezi kumuachia mpaka amalize mradi huu, tayari amechukua fedha zaidi ya asilimia 62 kwenye Bilioni 95″. Amesema Aweso

Naye Msimamizi wa Mradi wa Maji, Chalinze – DAWASA, Mhandisi Modesta Mushi amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 78, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo la mtambo, ujenzi wa matenki kufikisha maji maeneo mbalimbali na ujenzi wa vitekeo maji 351 maeneo mbalimbali katika eneo la mradi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter