Home VIWANDAMIUNDOMBINU Daladala kusaidia mwendokasi

Daladala kusaidia mwendokasi

0 comment 143 views

Baada ya kufanya ziara katika kituo cha mabasi ya mwendokasi eneo la Kivukoni jijini Dar es salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameagiza mabasi kumi ya kawaida, maarufu kama daladala kuongezwa kuongezwa katika usafiri wa mabasi yaendayo kasi ili kupunguza tatizo kubwa la usafiri.

Jafo ameagiza hayo baada ya kufanya mazungumzo na abiria kuhusu changamoto wanazokumbana nazo katika usafiri wa mwendokasi. Waziri huyo amekiri kusuasua kwa usafiri huo na kusema umekuwa ukileta usumbufu kwa wananchi na hadi kufikia sasa, hajaona hatua zozote zinazochukuliwa na watoa huduma.

“Tatizo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kituo cha mabasi cha Kimara wakati wa asubuhi na Kivukoni na Gerezani wakati wa jioni. Imeonekana pia kuna wakati mabasi yanaonekana yakisafiri tupu au yakiwa yameegeshwa pembeni mwa vitu, huku abiria wakiwa wamejazana katika vituo vya mabasi”. Amesema Waziri Jafo na kuongeza:

”Kutokana na hali hiyo namuelekeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (Dart), Mhandisi Ronald Lwakatare, ahakikishe angalau mabasi 10 ya Feeder Road maarufu kama Bomberdier yanayobeba abiria kutoka Mbezi kwenda Kimara Mwisho yahamishiwe katika barabara ya mwendokasi. Matano yawe yanabeba abiria wa Kivukoni na matano mengine yabebe abiria wa Gerezani”.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter