Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Kujiajiri kama umeajiriwa inawezekana

Kujiajiri kama umeajiriwa inawezekana

0 comment 59 views

Watu wengi hasa wale ambao wameajiriwa huchukulia suala la kujiajiri kuwa ni jambo rahisi. Dhana hiyo imepelekea wengine kuchukua maamuzi yasiyo sahihi ya kuacha kazi na kwenda kujiajiri bila kutafakari na kutengeneza mipango itakayowaelekeza katika safari yao ya ujasiriamali. Siku zote, watu wanawaza njia mbadala za kuweza kujiongezea kipato. Swali muhimu unalotakiwa kujiuliza ni Je, unaweza kujiajiri ili hali umeajiriwa?

Kama jibu lako ni ndio, basi tumia muda wako kuzingatia yafuatayo:

Kwanza kuwa mwepesi wa kujifunza. Inaweza kuwa kupitia makosa yako au hata ya wengine. Kabla ya kujiajiri, jifunze kupitia makosa yaliyofanywa na wale wanaokuzunguka kisha andaa mkakati mbadala kutatua makosa hayo. Baada ya hapo orodhesha namna utakavyoweza kuikuza biashara hiyo na kiasi ambacho utaweza kutumia kuendeleza biashara yako.

Fanya uchunguzi. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa kina kuhusu biashara unayotaka kuanzisha. Hii itakusaidia kujua wapinzani  na washindani wako na inakuwezesha kufahamu kama utaweza kuwamudu na kwa mbinu zipi. Fanya utafiti, kuwa mdadisi. Uchunguzi utakusaidia kujua kama biashara hiyo au huduma hiyo itakuletea maendeleo zaidi au la.

Baada ya kupata taarifa kamili kuhusu biashara au huduma unayotarajia kuwekeza. Tengeneza nyaraka ya mwisho ambayo itatoa maelezo husika kwa lugha inayomvutia msomaji. Nyaraka hiyo hufahamika zaidi kama ‘Proposal’. Baada ya kuitengeneza fikiria, Je unaweza kutumia fedha zako kuwezesha mradi huo? Kama ndio basi nyaraka hizo zinaweza kukusaidia hapo baadae ikitokea unahitaji mtaji mkubwa zaidi.

Fedha ikipatikana, basi unakuwa uko tayari kuchukua hatua ya kuanzisha biashara au huduma ya chaguo lako. Mwanzo siku zote huwa ni mgumu, usikate tamaa kwa kuachana na biashara hiyo  pale mambo yanapoenda tofauti na mipango yako. Tafuta njia mbadala ili baadae ujisifu kuwa ulibadili wazo kuwa fedha. Jambo la muhimu kuzingatia hapa ni  kwamba unatakiwa kuendelea na ajira yako hadi pale biashara yako itakaposimama yenyewe kwa asilimia mia moja.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter