Home VIWANDAMIUNDOMBINU Hakuna fidia waliobomolewa nyumba Mbezi, Kimara-JPM

Hakuna fidia waliobomolewa nyumba Mbezi, Kimara-JPM

0 comment 135 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema wananchi waliobomolewa nyumba ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka eneo la Kimara hadi Mbezi jijini Dar es Salaam hawatapatiwa fidia kwa sababu walijenga katika eneo la hifadhi ya barabara. Rais Magufuli amesema hayo leo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo inayofanyika eneo la Kimara Stop Over na kusisitiza wananchi wanalioathirika na upanuzi huo hawatopata faida hata wakienda mahakamani.

“Niwambie tu wananchi kuwa ukisogelea barabara madhara yake ni umasikini, hata mimi sijafurahishwa na hii bomoa bomoa kwa kuwa wapo ndugu zangu nyumba zao zimebomolewa. Ni vyema kuwaambia ukweli kesi hii hata wakienda wapi hawawezi kushinda”. Amesema Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter