Home AJIRA Ajira kupitia viwanda zaongezeka

Ajira kupitia viwanda zaongezeka

0 comment 80 views

Ofisa Mwandamizi wa Uchumi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Genoveva Kilabuko amesema mchango wa ajira kupitia sekta ya viwanda umeongezeka kutoka ajira 267,524 mwaka 2016 hadi 280,899 mwaka 2017. Kilabuko amesema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viwanda vya Chemi and Cotex kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Joseph Buchweishaija. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa kwa mwaka 2017 ni asilimia 5.5, ikiwa ni ukuaji mzuri ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwaka 2016.

“Serikali ya awamu ya tano imekuja na mpango wa Blueprint kwa ajili ya kurahisisha mazingira ya kufanya biashara”. Amesema Ofisa huyo.

Mbali na hayo, Kilabuko ameeleza kuwa mafanikio yaliyopatikana kupitia uzalishaji ni dalili nzuri kwa serikali pamoja na wadau mbalimbali kuwa, nchi ipo katika hatua sahihi za kufikia azma ya muda mrefu ya maendeleo.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa viwanda hivyo amesema wameajiri wafanyakazi takribani 1,500 katika viwanda vyao na asilimia 65 ya waajiriwa ni wanawake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter